Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Kutana na Familia Inayoishi Makaburini Dar kwa miaka 7 sasa





Makala: Waandishi Wetu | Gazeti la Uwazi, Toleo la Desemba 20, 2016


Dar es Salaam: Unaweza kudhani ni simulizi ya mambo ya kusadikika, lakini ni ukweli mtupu, suala hili linatokea katika ulimwengu huu, tena katika Mitaa ya Ubungo-Maziwa jijini hapa, ambapo familia ya Rasta Magoda na Amina Robert inaishi katika eneo la makaburi yanayolizunguka eneo hilo, yapata miaka saba sasa.

Katika makala haya, waandishi wa Uwazi, Boniphace Ngumije, Ally Katalambula na Meckion Mathiew wanakuletea historia, sababu ya familia hiyo kuishi katika eneo hilo, mauzauza na mambo mengine mengi ambayo familia hiyo imeweza kushuhudia kwa muda wote huo wa miaka saba ikiwa hapo baada ya kuitembelea katika makazi yao hayo.

Rasta Magoda akiwa na mwanaye.

Akizungumza na Uwazi kwa kujiachia, Rasta Magoda ambaye ni baba wa familia hiyo anasema kuwa alianza kuishi hapo mwaka 2009 baada ya kupata ajali ya gari iliyomsababisha kuwa mlemavu wa mguu na kushindwa kufanya shughuli kubwa za kujipatia kipato zaidi ya kazi ndogondogo.

“Si kwamba ninapenda kuishi mahali hapa (Makaburi ya UFI yaliyopo Ubungo-Maziwa, Dar) mimi na familia yangu. Lakini hii ni baada ya kupata ulemavu na kujikuta siwezi kufanya kila kitu kwa ajili ya kujipatia kipato.

“Kipindi cha nyuma nilikuwa dereva wa magari lakini mwaka 2006, nilipata ajali. Nilipopona, mwaka 2009 katika namna ya kujitafutia kipato niliamua kuhamia katika eneo hili,” anasema Rasta Magoda.

Mwandishi: Kwani wewe ni mwenyeji wa wapi?

Rasta Magoda: Tanga.

Mwandishi: Kipindi unaanza kuishi hapa katika eneo hili la makaburi hukuwa unaogopa?

Mke wa Rasta Magoda akiwa na wanaye.

Rasta Magoda: Hapana, kwanza unatakiwa kufahamu kuwa wakati ninaanza kuishi hapa, haya makaburi hayakuwepo (yalikuwepo lakini hayakuwa yamekaribia au kuwa jirani na kibanda anachoishi), yamekuja baadaye, yaani yamenikuta.

Mwandishi: Kwani eneo hili ulipewa na nani?

Rasta Magoda: Eneo hili nililipata kutoka kiwanda cha jirani lakini sipendi kukitaja jina moja kwa moja.

Mwandishi: Hujawahi kupata usumbufu wowote kutoka serikalini au mtu yeyote kuhusu kuishi hapa?

Rasta Magoda: Usumbufu ambao nimewahi kupata ni kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa kipindi fulani hivi, alikuwa hataki niishi hapa, lakini baadaye nilikwenda kwa mtendaji nikazungumza naye vizuri na kumuomba aniachie hapa maana ni sehemu naitumia kujiingizia kipato na kupata riziki, akaniruhusu kuishi hapa.

Mwandishi: Kwa hiyo umeoa huku unaishi hapahapa?

Rasta: Ndiyo.

 
Mtoto wa Rasta Magoda akiwa katika pozi.

Mwandishi: Swali kwa mama, wewe ni mwenyeji wa wapi na ulichukuliaje siku ya kwanza ulipoletwa na mumeo kuja kuishi hapa?

Amina: Mimi ni mwenyeji wa Kasulu, Kigoma, nilipachukulia kawaida tu, maana niliamua mwenyewe kuja kuishi na mume wangu na pia hali yake nilikuwa naifahamu.

Mwandishi: Siyo kwamba alikushawishi kwa namna yoyote na ukajikuta upo hapa?

Amina: Hapana, niliamua mwenyewe.

Mwandishi: Ndugu zenu huwa wanawatembelea mkiwa katika eneo hili?

Amina: (Akicheka), ndiyo kwa nini wasije?

Mwandishi: Inawezekana wakawa wanaogopa kutokana na eneo lote kuzungukwa na makaburi?

Amina: Hapana. Hapa hii ni sehemu salama kabisa na hata wakija huwa tunawaondoa wasiwasi.

Mwandishi: Watoto wenu hawa wote wawili mmewapata mkiwa hapahapa?

Amina: Ndiyo, tulikuwa hapahapa, huyu mkubwa anaitwa Chris na mdogo Robert.

Mwandishi: kwa upande wa malezi kwa watoto unakutana na changamoto gani kama mama, tukiangalia pia katika eneo hili hakuna hata watoto wengine wanaoweza kucheza nao, kuna shida gani mnakutana nayo.

Amina: Hakuna changamoto yoyote, kama ni watoto kucheza mimi nacheza nao na kwetu malezi ni mazuri tu.

Mwandishi: Hakuna wakati watoto mnawakuta wakiwa juu ya makaburi wakicheza wakati mwingine?

Amina: Hapana, watoto wanachezea hapahapa katika maeneo ya nyumba tu.

Mwandishi: Tukirudi kwa rasta, mnategemea kuishi hapa mpaka lini?

Rasta Magoda: Mpaka pale Mungu atakaponisaidia kupata kipato kizuri na kujimudu vizuri kimaisha.

Amissi Tambwe wa Yanga ampasua kichwa kocha Simba SC




Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Hamis Tambwe.

INGAWA Simba bado ni ya mwendokasi katika kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, lakini benchi la ufundi haliridhishwi na kiwango cha safu ya ushambuliaji kwani wameendelea kutegemea nguvu ya safu ya kiungo kusaka pointi tatu, tofauti na Yanga ambao washambuliaji wake chini ya Amissi Tambwe wanafanya vizuri. Ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Ndanda uliwarejesha kileleni Wekundu wa Msimbazi kwa pointi 38, pointi mbili mbele ya Yanga kwa mabao ya viungo Mzamiru Yassin na Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’ lakini benchi hilo linaona kuwa wana kazi kubwa ya kufanya.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ‘Mia Mia’, amesema hawafurahishwi na mwenendo wa mafowadi wao kwani hakuna aliye juu kwenye chati ya ufungaji zaidi ya kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya anayeongoza kwa mabao tisa sawa na Simon Msuva wa Yanga. Katika chati hiyo, Tambwe anawafuatia kwa mabao saba sawa na fowadi Rashid Mandawa wa Mtibwa Sugar huku fowadi tegemeo wa Simba, Fredric Blagnon akiwa amefunga bao moja, Ibrahim Ajibu ‘Cadabra’ ana mabao matatu na Laudit Mavugo amefunga matano tu. “Huwezi kufurahia kama unaona kwenye chati ya juu hakuna straika wako, hakuna mwenye mabao saba kulinganisha na wengine kama Kichuya na Tambwe kwenye chati ya wafungaji.


“Angalia ni mechi ngapi hakuna straika wetu amefunga bao? Kweli ni jambo ambalo bado kama benchi la ufundi linatuumiza akili na ndiyo maana utaona tunafanya kila jitihada kuhakikisha tunaiboresha safu ya mbele kama wenzetu. “Hiyo ni tofauti na Yanga kwani Tambwe mara ya mwisho alifunga mechi tatu zilizopita, raundi ya 13 wakati wakiichapa Mbao mabao 3-0 kabla ya Donald Ngoma kufunga raundi ya 14 kwenye kichapo cha mabao 2-1 mechi dhidi ya Mbeya City ugenini, hawa wanatufanya tuumize sana kichwa kwa kuwa mabao mara nyingi yanafungwa na viungo.”

Mpyaa kabisa...Hawa ndio watu 20 maarufu duniani wenye mashabiki wengi zaidi Facebook...List nzima iko hapa



Leo December 20, 2016 kupitia FANPAGELIST wametoa list ya mastaa 20 wakiwemo wanasoka, wacheza filamu na mastaa wa muziki wanaoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi zaidi duniani, list hiyo imeongozwa na mwanasoka staa Cristiano Ronaldo anayeichezea club ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno.

Ronaldo amewapita mastaa wakubwa wa muziki akiwemo Justin Bieber ambaye ameshika nafasi ya 7 wakati mpinzani wake mkubwa kwenye soka Lionel Messi ametajwa kwenye nafasi ya 5, staa mwimbaji Rihanna ameshika nafasi ya 6 na staa muigizaji na muimbaji Selena Gomez ambaye anaongoza kwa kuwa mashabiki wengi zaidi Instagram, huku ameshika nafasi ya 17.

Full List nimekuwekea hapa.

Ujumbe wa Ronaldinho kwa Cristiano Ronaldo baada ya ushindi wa Ballon d’Or



Jumatatu ya December 12 2016 ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo, staa huyo wa Ureno December 12 ndio siku rasmi aliyotangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or 2016.

Baada ya ushindi huo wa tuzo ya nne ya Ballon d’Or, staa wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho ambaye amewahi kushinda tuzo hiyo mwaka 2005, ametumia ukurasa wake wa instagram kumpongeza Ronaldo kwa ushindi huo, Ronaldinho ametumia lugha ya kireno.





“Hongera rafiki yangu Cristiano kwa ushindi wa tuzo hiyo ulistahili na kwa miaka ya hivi karibuni umekuwa na mafanikio makubwa, tuzo hiyo ni heshima kwa manufaa yako”

 

Copyright © 2013. MKOGELO JR - Haki zote zimehifadhiwa